The House of Favourite Newspapers

Mapinduzi Ya Huduma za Vikundi Kidijitali Tanzania – Video

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi akishirikiana na viongozi wengine kuonesha jarida la M-Koba wakati wa hafla ya kuzindua huduma ya M-Koba, huduma ya kwanza na ya kipekee nchini kwa ajili ya vikundi vya kuweka akiba nchini Tanzania. Wengine ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kati), Mkuu wa M-Commerce Vodacom, Epimack Mbeteni (wapili kushoto) na Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB Kolimba Tawa (L).

 

VODACOM kwa kushirikiana na TPB Benki wamekuletea huduma mpya  ya kutunza fedha, kupeana mikopo na kugawana faida kwa vikundi kama familia na marafiki, VICOBA, VSLA, UPATU na vikundi mbalimbali vyenye utamaduni wa kuchanga kwa lengo la kuweka akiba na kukopeshana pesa. Huduma hii inaitwa M-KOBA.

 

M-KOBA ni huduma mpya ya kuchanga Kidigitali inayoleta usalama0 wa fedha za wanakikundi, uwazi na urahisi wa kuchanga kutoa popote kupitia mtandao wa Vodacom M-pesa.

 

 

M-KOBA Imeletwa ili kutatua changamoto mbalimbali ambazo Vikundi vinakutana nazo katika mfumo wa kutumia pesa taslim kama usalama mdogo wa fedha zinazokusanywa, wanavikundi kutokuwa urahisi wa kukusanya pesa.

Piga *150*00# > chagua HUDUMA ZA KIFEDHA > Chagua M-KOBA.

Kwa maelezo zaidi na msaada zaidi kuhusu huduma ya M-KOBA piga huduma kwa wateja namba 100 bure wakati wote.

Comments are closed.