Mapishi ndiyo limbwata kuu kwa mumeo

szechuan spicy chix 3Asalam Alaikum, Bwana Yesu Asifiwe, bila shaka wazima wa afya kama nilivyo, nina amani kwa sababu nimempigia kura yule ninayeamini anafaa kuliongoza taifa hili.

Leo nimekuja na mada nyepesi kwa muonekano lakini ni mada kali na ina mapana zaidi kwani ndoa nyingi siku hizi zinavunjika kwa sababu ya wanawake kutojua kupika.

DSC01401Kwa nini mumeo akapikiwe na kimada?

Naomba nikufundishe jinsi ya kutumia mapishi kama limbwata ambapo mumeo itamlazimu kurudi nyumbani akikumbuka tu jinsi unavyompikia.

Nimekuwa mfundaji kwa miaka mingi na siku hizi vilio vya mabiharusi wengi ni kutojua kupika. Huyu naye ni mmoja kati yao ambapo alinitafuta baada ya kuingia kwenye ndoa, hebu msikie;

20141217_221226“Mama nilipomaliza darasa la saba nilipelekwa shule ambayo ni ya bweni, sikubahatika kujifunza jinsi ya kupika, baada ya hapo nikaenda chuo na sasa nimebahatika kupata mume, kwa jinsi nilivyokaa naye kwa muda mchache ni mtu ambaye ana hobi ya kupika sasa nifanyeje mimi sijui kupika?” Huyu ni mwari ambaye nilimfunda baada ya kuingia kwenye ndoa akakutana na changamoto ya mumewe kupenda kula vyakula vya aina tofauti.

loversKwa mfano huu mdogo bila shaka umenielewa, sasa naomba nikueleze tu mume anataka ratiba ya mlo kama alivyo mtoto na unachotakiwa ni kuifuata vilivyo.

Nimekaa kwenye ndoa kwa muda mrefu, mume wangu huwa namfanya kama mtoto kwani ana ratiba yake na hata akienda wapi anajua lazima apate mlo kwa mkewe ambao umekamilika kwa kila idara.

Asubuhi amka mwanamke jipange siyo ukanunue mkate dukani hebu muulize mumeo angependa umpikie nini kwa ajili ya kifungua kinywa? Lakini pia mshauri ale nini ili mwili uwe na nguvu siku nzima.

Kama ni mfanyakazi jitahidi kumuandalia mapema chakula cha mchana lakini cha usiku si lazima ukipike wewe, kiandae kwa maana ya kujua mumeo atakula nini kama una muda ingia mwenyewe jikoni.

Wasiojua kupika

Bibi kama hujui kupika nikushauri tu ujifunze, ingia mitandaoni, soma  kwenye majarida ya mapishi au tafuta wanawake wanaojua kupika wakufundishe kwani asikwambie mtu mapishi ni limbwata tosha kwa mumeo siyo mpaka uende kwa mganga kwani dawa zikiisha atarudi palepale lakini mapishi ndiyo mwisho wa reli Kigoma.

Faida ya mtu kumpikia mumewe

Faida ya mtu kumpikia mumewe ni pamoja na kumpa afya njema na kumfanya awe shupavu faragha.

Kwa leo naomba niishie hapa.


Loading...

Toa comment