The House of Favourite Newspapers

MAPISHI YA LEO MKATE WA TAMBI

LEO kwenye safu hii ya mapishi tunajifunza jinsi ya kupika mkate wa tambi ambao una ladha nzuri na rahisi kuutengeneza.

MAHITAJI

-Tambi pakti moja

-Tui la nazi kikombe kimoja

-Sukari nusu kikombe cha chai

-Maziwa ya unga nusu kikombe

-Samli kijiko kimoja cha supu

-Zabibu robo kikombe

-Iliki robo kijiko cha chai

KUTAYARISHA NA KUPIKA

Katakata tambi kisha zichemshe kidogo tu katika maji yanayochemka na uzichuje (zisiive sana).

Chukua tui la nazi lichemshe, pamoja na vitu vyote vingine, koroga vicha-ngan-yike katika moto.

Weka tambi kisha koroga vizuri ziache ziive.

Chukua samli paka kwenye kikaango chako cha kupikia chenye shimo kisichokuwa na mkono au tumia trei ya keki iliyo nzito.

Tambi zikikaribia kukauka, mimina katika kikaango au trei ya keki.

Didimiza kwa mwiko kuzisawazisha zijifunge katika duara.

Ukishafanya hatua hiyo, paka samli kidogo juu yake.

Baadaye choma katika oven au jiko la mkaa lenye moto wa wastani.

Acha kwa dakika 20 hadi zikauke na zianze kubadilika rangi.

Zima moto wa chini kisha washa au weka moto wa juu kidogo tu ziweze kuwa na rangi ya hudhurungi.

Zikishabadilika rangi na kukauka vizuri, epua kisha zitoe katika kikaango kisha ziweke kwenye sahani.

Hapo zitatoka kama mkate, kata vipande tayari kwa kula.

 

Gladness Mallya | +255 654 880707

Comments are closed.