Mapya! Shamsa Ford Amlipua Nicole ‘Awalipe Watu Pesa Zao’ – Video
Mwanadada mrembo kwenye tasnia ya uigizaji na mfanyabiasha wa nguo za kike, Shamsa Ford amefunguka na kueleza kuwa wakati alipokuwa anaachana na Rapa maarufu Bongo nchini, Nay wa Mitego hawakuachana kwa ubaya. Pia ameshangazwa na sakata la Joyce Mbaga, maarufu kama Nicole Berry, ambaye anashutumiwa kwa kupokea kiasi cha Shilingi milioni 185.5 kutoka kwa umma bila kupata kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT).