The House of Favourite Newspapers

16 Wafariki Magari Mawili ya Abiria Yakigongana, Kuwaka Moto Tarime

  WATU 16 wamefariki dunia baada ya kuteketea kwa moto kufuatia ajali mbaya iliyotokea jana katika eneo la Komaswa maarufu kama Kwa-Gachuma lililopo wilayani Tarime mkoani Mara ambapo magari mawili ya abiria aina ya Toyota Hiace kugongana uso kwa uso na kuteketea kwa moto.

Miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo itazikwa katika eneo ilipotokea ajali hiyo .

Akizungumza leo Jumanne Novemba 27, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima,  amesema uamuzi huo umechukuliwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kutokana na ushauri uliotolewa na Kamati ya Taifa ya Maafa.

Amesema hadi sasa majina 12 kati ya 16 ya waliofariki dunia yamejulikana licha ya miili yao kutotambulika kutokana na jinsi ilivyoungua.

“Ni miili miwili tu ambayo ilitambuliwa ukiwemo wa dereva na mwingine uliotambulika baada ya kukutwa na cheni shingoni,” amesema Malima.

 

Amesema mazishi hayo yatafanyika kesho Novemba 28, 2019 saa nne asubuhi, kwamba mabaki yaliyotokana na miili kuungua yatakusanywa na kuzikwa eneo hilo.

Amesema baada ya mazishi eneo hilo utajengwa mnara kwa ajili ya kumbukumbu.

Comments are closed.