The House of Favourite Newspapers

ads

Marcus Rashford Awaita Mezani Man United Majadiliano juu ya Mkataba Mpya

0
Marcus Rashford

MANCHESTER United na Marcus Rashford wanaripotiwa kuendeleza majadiliano juu ya mkataba mpya na klabu hiyo ambayo inaaminika kuwa wanataka kumpa mkataba mrefu na bora zaidi ya alionao sasa.

Rashford, 25, amekuwa kwenye kiwango bora siku za hivi karibuni katika klabu hiyo. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amefunga mabao 16 katika michuano yote, ikiwa ni pamoja na mechi za mwisho dhidi ya Liverpool, Arsenal na Manchester City kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Hata hivyo, Manchester Evening News na The Sun sasa zinaripoti kwamba klabu hiyo ina nia ya kutaka kumpa ujasiri zaidi kwa kumpa mkataba mpya.

Baada ya kuzorota kwa kiwango cha Rashford hasa msimu uliopita, kilizuia tetesi kuwa huenda mshambuliaji huyo anaweza kuuzwa kwenye timu hiyo. Na sasa hadithi ni tofauti.

PSG, ni moja kati ya timu ambayo ilikuwa inatajwa sana, kuwa staa huyo angejiunga nayo kama angeondoka United.

ORUMA – “CHAMA SIYO MKUBWA KULIKO SIMBA, VIONGOZI WAANGALIE kwa UPANDE wa KOCHA”…

Leave A Reply