The House of Favourite Newspapers

Marehemu Chadwick Ashinda Tuzo ya Golden Globe

0

Chadwick Boseman alishinda tuzo yake ya kwanza ya Golden Globe katika filamu ambayo hakuishi kuiona.

 

Mjane wa nyota huyo Taylor Simone Ledward, alikubali tuzo hiyo ya muigizaji bora kwa niaba ya muigizaji huyo , ambaye alifariki dunia mwezi Agosti kutokana na saratani ya utumbo akiwa na umri wa miaka 43 – miezi mitatu kabla ya filamu kwa jina ‘’Ma Rainey’s Black Bottom’’ kuzinduliwa.

 

 

‘’Angesema kitu kizuri chenye msukumo , kitu ambacho kingepaza ile sauti ndogo ndani yetu sote inayosema unaweza’’, alisema Simone Ledward, huku yeye na waliohudhuria wakijifuta machozi.

 

‘’Hilo linakwambia endelea, hilo linakuita na kukurudisha katika kile ambacho unapaswa kufanya wakati huu katika historia’’.

 

Boseman ni mtu mweusi wa kwanza katika orodha hiyo katika kipindi cha miaka 15. Forest Whitaker alishinda katika sherehe ya 2007 kwa kuigiza kama Idi Amin ‘’the Last king of Scotland’’.

 

 

Tuzo hiyo pia inamfanya Boseman kuwa mtu mweusi wa kwanza aliyefariki kushinda tuzo hiyo katika orodha ya uigizaji.

 

 

Boseman alikuwa maarufu katika filamu ya michezo ya ’42’ ya mwaka 2013 kuhusu ubaguzi aliofanyiwa mchezaji wa kulipwa wa besiboli Jackie Robinson na ile ya ‘Get on Up’ mwaka 2014 kuhusu maisha ya mwimbaji wa nyimbo aina ya soul James Brown.

 

 

Nyota huyo, Boseman, aliigiza kama mtawala wa Wakanda, filamu iliyoangazia Afrika ya kufikirika yenye teknolojia zilizoendelea sana za kisasa.

Leave A Reply