The House of Favourite Newspapers

Marekani: Biden Amteua Kamala Mgombea-Mwenza

0

JOE BIDEN ambaye anayegombea urais wa Marekani kupitia Chama cha Democrat amemteua Kamala Harris kuwa mgombea-mwenza katika uchaguzi mkuu wa Novemba 2020.

 

Kamala (55) ambaye ni Seneta wa Jimbo la California alikuwa miongoni mwa wanachama wa Democrat walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea urais.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa mwanamke mweusi kuteuliwa nafasi hiyo ya juu katika historia ya siasa za nchini Marekani.

 

Uteuzi wa Kamala unaashiria Biden anakubali wapiga kura weusi wana nafasi kubwa katika uchaguzi huo ambapo atapambana na Rais Donald Trump.

 

Leave A Reply