The House of Favourite Newspapers

Marekani Imeitungua Ndege ya Jeshi la Syria

0
Marekani imeitungua ndege ya kijeshi ya Syria iliyokuwa ikijiandaa kuwashambulia wanamgambo wa IS ambao wamekuwa wakihatarisha maisha ya wananchi wa nchi hiyo huku umoja wa mataifa ukitaka kuwepo na usuluhishi.
Aidha, Marekani imesema kuwa imefikia hatua hiyo mara baada ya jeshi la Syria kuvishambulia vikosi vya Syrian Democratic Force SDF, vinavyoungwa mkono na MarekaniĀ  kwa lengo la kupambana na wanamgambo wa Islamic State.
Kwa upande wa Serikali ya Syria imesema kuwa ndege yake ilikuwa katika maandalizi ya kuwashambulia wanamgambo wa Islamic State na si vikosi vya Syrian Democratic Force vinavyoungwa mkono na Marekani.
Vikosi vya Syrian Democratic Force (SDF ) vinaungwa mkono na umoja unaoongozwa na Marekani kwaajili ya kupambana na wanamgambo wa Islamic State ambao wamekuwa tishio katika ukanda huo.

Yaliyojiri Bungeni Mjini Dodoma Leo Jumatatu Juni 19

Nishushe Idd Mosiā€¦ Roma Atawaongoza Wakali Hawa Kuliamsha Dude, Dar Live

Leave A Reply