The House of Favourite Newspapers

Marekani Kununua Mfumo wa Israel wa Kujilinda Dhidi ya Makombora

JESHI la Marekani limetangaza mipango ya kutaka kununua mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora wa Israel ambao unafahamika kwa jina Iron Dome. Mfumo huo unaotumia rada na kutungua makombora kwa lengo la kukabiliana na tishio lolote umekuwepo tangu mwaka 2011.

 

Idara ya ulinzi nchini Marekani imesema kuwa mfumo huo utatumika kufanya majaribio huku ikitafuta mahitaji ya muda mrefu ya jeshi lake.

”Hili ni dhihirisho jingine la kuimarika kwa ushirikiano wetu thabiti na Marekani, na onyesho kwamba Israel inazidi kupandisha hadhi yake duniani,” taarifa yake iliendelea.

 

Ufanisi Wake
Mfumo huo wa Iron Dome hufanya kazi kwa kufuatilia tishio lolote la shambulio kwa muda mfupi kupitia rada yake, kisha inachambua data kuhusu eneo litakaloathirika – kabla ya kuamua kurusha kombora litakalotungua shambulio hilo.

Maofisa wa Israel wanasema kuwa mfumo huo wa makombora unaoweza kufanya kazi katika mazingira yoyote mbali na kusafirishwa kutoka eneo moja hadi jingine una mafanikio ya hadi asilimia 90.

Unasemekana kuwa na uwezo wa kulinda mji mzima dhidi ya tisho lolote la angani na umetumiwa sana kutungua makombora yaliyorushwa na wapiganaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.

 

Utengenezaji wa mfumo huo

Ilichukua miaka kadhaa kuunda mfumo huo na ulitengezwa na kampuni ya ulinzi nchini Israel ya  Rafael Advanced Defence Systems.

Marekani ilichangia sana katika uundaji wa mfumo huo, na baadhi ya vifaa vyake vinatoka kwa makampuni ya Marekani. Katika taarifa, idara ya ulinzi nchini Israel ilisema kuwa ununuzi huo ulifanyika kutokana na mahitaji yake ya dharura ya jeshi la Marekani.

 

Ripoti zilivuja kuhusu ununuzi huo mwezi uliopita.

Kanali Patrick Seiber wa jeshi la Marekani amesema kuwa mfumo huo unachunguzwa na kujaribiwa ili kuwalinda wanajeshi wa Marekani walio katika mataifa ya kigeni.

 

Huku mfumo huo wa Iron Dome ukiwa umetumika na wanahewa wa Israel tangu mwaka 2011 na kuthibitisha uwezo wake katika vita, lazima ibainike kuwa jeshi la Marekani litauchunguza kwa lengo la kuimarisha uwezo wake wa siku zijazo wa kujilinda, taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano ilisema.

Alichokisema RC Makonda Baada ya Kukagua Standard Gauge

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.