The House of Favourite Newspapers

Marekani kutoa Mil.17 kunufaisha wavuvi wa Ukanda wa Bahari

1.Fatma Sobo (katikati0 akisoma taarifa yake kwa wanahabari (pichani hawapo).Fatma Sobo (katikati) akisoma taarifa yake kwa wanahabari (hawapo pichani).
3.Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
4.Wanahabri wakifuatilia mkutano huo.Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

WAVUVI wa Ukanda wa Bahari watanufaika na Mradi wa Udhibiti wa Uvuvi na Malengo Shirikishi wenye thamani za dola milioni 36 za Marekani kupitia mradi wa uvuvi wa ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi unaojulikana kama ‘South West Indian Ocean’ (SWIOFISH).

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Judith Mhina, amesema mradi huo utatekelezwa ndani ya miaka sita kwa awamu tatu ambapo umelenga kuimarisha usimamizi madhubuti wa uvuvi katika ngazi ya kanda, kitaifa na kijamii ambapo hapa nchini utasaidia kwenye ukuzaji na utunzaji wa viumbe wa baharini.

Amesema mradi huo utafanya utafiti wa kujua mahitaji halisi ya wadau kwenye mradi huo huku ukipitia muongozo wa uwekezaji katika ukuzaji viumbe baharini, ikiwa na lengo la kuwawezesha wawekezaji kufahamu taratibu za kutafuta uwekezaji kwenye maeneo hayo.

Vilevile amesema kuwa mradi huo utasaidia kukomesha uvuvi haramu wa kutumia mabomu na wavu bandia kwa kushirikisha Wizara ya Maliasili na Utalii na wizara nyingine.

Mhina ametaja mashirika yaliyochangia fedha kusaidia mradi huo kuwa ni Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) uliochangia milioni 5,000,000, za Marekani, Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo (IDA) uliochangia milioni 31,000,000 ambapo jumla ya fedha zote zilizochangiwa ni milioni 36,000,000, ambapo Tanzania bara ilipatiwa shilingi milioni 17,280,000, na visiwani shilingi milioni 11,520,000, na Mamlaka ya Usimamizi wa Uvuvi katika Bahari Kuu ilipewa shilingi 7,2000,000.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

Comments are closed.