WATAALAM wa Usalama Mtandaoni nchini Marekani wameishutumu China kuwa inajaribu kudukua taarifa kuhusu tafiti zinazofanya za #COVID-19.
Shirika la upelelezi nchini Marekani (FBI) na Idara ya Usalama imepanga kutoa onyo kwa Wachina wanaoshutumiwa kudukua taasisi za afya zinazofanya tafiti kugundua chanjo ya #CoronaVirus.
Aidha, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya #China, Zhao Lijian, amekanusha madai hayo akisema China iko thabiti katika kupinga uhalifu wote wa kidijitali.




