Marekani Yasema Tanzania Ni Salama Kutembelea

IDARA ya Ushauri wa Afya ya Marekani imeitaja nchi ya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi salama ambazo wananchi wake (Wamarekani) wanaweza kuitembelea katika majira haya ya joto.

 

Taarifa iliyotolewa na idara hiyo na kutangazwa na kituo cha Televisheni cha CNN, imesema wananchi wake wanaweza kuitembelea Tanzania lakini wakifika lazima wafanye vipimo vya Covid-19 kabla ya kuendelea na shughuli zao.

 

Hivi karibuni Serikali ya Tanzania kupitia kwa Rais  John Magufuli  ilifungua milango kwa watalii kutoka nchi mbalimbali kuja kuitembelea na kwamba ugonjwa wa Covid-19 umedhibitiwa hapa nchini lakini ni vyema wananchi na wageni kuendelea kuchukua tahadhari.

 

Wamarekani wanaruhusiwa kuingia kwenye nchi hizi bila masharti:

 • Albania
 • Dominican Republic
 • Kosovo
 • Maldives
 • Mexico
 • North Macedonia
 • Serbia
 • Tunisia
 • Turkey

Wamarekani wanaruhusiwa kuingia kwenye nchi hizi kwa masharti ya kupima Covid-19.

 • Antigua and Barbuda 
 • Aruba 
 • Barbados 
 • Belize 
 • Bermuda 
 • Cambodia 
 • Croatia 
 • Dominica 
 • Ecuador 
 • Egypt 
 • French Polynesia 
 • Ireland 
 • Jamaica 
 • Rwanda 
 • St. Barts 
 • St. Lucia 
 • St. Maarten 
 • St. Vincent and Grenadines 
 • Tanzania 
 • Turks and Caicos 
 • Ukraine 
 • United Arab Emirates 
 • United Kingdom 

Toa comment