Marekani Yasaidia Israel kuyadungua Makombora ya Iran
MAREKANI usiku wa kuamkia leo Oktoba 2, 2024 imetungua makombora ya masafa marefu ya Iran yaliyofyatuliwa nchini Israel, Pentagon imesema.
Jeshi la Israel limesema takriban makombora 180 yalirushwa dhidi ya Israel, huku mengi yakizuiliwa angani.
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ametetea mashambulio hayo akiyaita majibu ya uamuzi katika kulinda maslahi ya Iran na raia.
Hakuthibitisha iwapo Marekani imetungua makombora yoyote ya Iran yaliyotumika katika mashambulizi hayo na aliongeza kuwa taarifa hizi bado hazijabainika.
Iran ilirusha makombora 180 kuelekea Israel, jeshi la Israel limesema.
Meja Jenerali Ryder aliongeza kuwa Pentagon haikuwa na taarifa ya tahadhari yoyote kuhusu shambulio hilo.
Rais Biden amesema Marekani inaunga mkono kikamilifu Israel baada ya shambulio la Jumatano.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Iran imefanya kosa kubwa usiku wa leo, na italipia.