The House of Favourite Newspapers

Marekani Yataifisha Jumba la Kifahari la Rais wa Zamani wa Gambia Yahya Jammeh

0
Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh.

 

WIZARA ya Sheria ya Marekani inasema imefanikiwa kutwaa jumba la kifahari lililonunuliwa na rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh kwa $3.5m (£2.7m) kwa madai ya mapato ya rushwa.

Mali hiyo iliyoko Potomac, Maryland, inasemekana kupatikana kupitia wakfu ulioanzishwa na mkewe, Zineb Jammeh.

 

Sasa limechukuliwa na Marekani pamoja na mapato yote ya kukodisha yanayotokana na mali hiyo tangu malalamiko yalipowasilishwa mnamo 2020, taarifa ya idara hiyo ilisema.

 

“Marekani inakusudia kuuza mali hiyo, na inapendekeza kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba mapato yatokanayo na mauzo ya mali iliyotwaliwa yatumike kuwanufaisha watu wa Gambia waliodhuriwa na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka ya Rais wa zamani Jammeh,” idara hiyo ilisema.

 

Rais huyo wa zamani anashutumiwa kwa kula njama na familia yake na washirika wake kwa kutumia makampuni ya ng’ambo na amana za ng’ambo kujipa mapato yake yanayodaiwa kuwa ya kifisadi duniani kote.

 

Serikali ya Gambia wiki hii ilisema iko tayari kumfungulia mashitaka kwa kile ilichokiita “mamia ya uhalifu” aliofanya wakati wa utawala wake.

EXCLUSIVE: KUTANA NA MZUNGU WA MWANANYAMALA ANAYETREND MITANDAONI, UTACHEKA VITUKO VYAKE…

Leave A Reply