The House of Favourite Newspapers

Marekani Yatishia Kuifungia TikTok Kisa Ofa ya Microsoft

0

RAIS wa Marekani, Donald Trump,  amesema kuwa atazuia mtandao wa TikTok usitumike nchini humo kufuatia kampuni ya China inayomiliki mtandao huo kukataa ofa ya Kampuni ya Microsoft inayotaka kuinunua TikTok.

 

Rais Trump amewaambia waandishi wa habari kuwa atatumia mamlaka ya dharura ya kiuchumi au amri ya serikali (executive order) kutekeleza azma yake hiyo.

 

Marekani inailazimisha kampuni ya ByteDance ya China inayomiliki TikTok kuuza shughuli za uendeshaji wa mtandao huo Marekani kufuati tetesi kuwa mtandao huo unaomilikiwa na kampuni iliyopo nje ya Marekani unaweza kuhatarisha usalama wa taifa.

 

Taarifa kutoka nchini Marekani zinaeleza kuwa Microsoft inafanya mazungumzo ya kuinunua TikTok, hata hivyo, kampuni hiyo haijasema chochote kuhusu taarifa hiyo.

 

Mtandao huo umeshika kasi duniani huku ukiwa mtandao wa kwanza wa China kuwa na watumiaji wengi zaidi nje ya nchi hiyo. Mtandao huo ulipakuliwa mara milioni 315 katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2020, ikiwa ni idadi kubwa zaidi katika historia kwa programu kupakuliwa ndani ya kipindi cha robo moja ya mwaka.

 

Baadhi ya watunga sera nchini Marekani wanahofu kuwa taarifa ambazo mtandao huo unakusanya kutoka kwa Wamarekani zinaweza kuishia mikononi mwa serikali ya China, licha ya kuwa mtandao huo kusisitiza kuwa unahifadhi taarifa zake nje ya China na hauwezi kukubali kuingiliwa na Beijing.

 

Kampuni hiyo imeeleza kuwa taarifa za raia wa Marekani zinahifadhiwa Marekani chini ya ulinzi mkali, huku wataalamu wa usalama mitandaoni wakisema mada kuwa TikTok inaweza kuhatararisha usalama wa taifa ni dhahania.

Leave A Reply