The House of Favourite Newspapers

Marekani Yatoa dola milioni 25 kwa atakayemkamata Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro

0
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro.

Leo Januari 11, 2025 imeripotiwa kuwa Marekani imetoa zawadi ya dola milioni 25 (zaidi ya Tshs bilioni 67 za Kitanzania) kwa atakayemkamata Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro.

Zawadi kutoka Marekani inataja mashtaka ya mihadarati na ufisadi yaliyoanzia 2020 kwani mwaka huo Marekani ilimshtaki Maduro, na maafisa wengine wakuu nchini kwa ugaidi wa mihadarati.

Iliwashutumu kwa kusafirisha Cocaine nchini Marekani na kutumia dawa hizo za kulevya kama silaha ya kudhoofisha afya ya Wamarekani.

Maduro amekanusha shutuma hizo.

Marekani pia iliweka tena vikwazo vya mafuta mwaka jana kwa Venezuela, baada ya kuvipunguza kwa muda kwa matumaini kuwa Maduro angeweza kuhamasishwa kufanya uchaguzi huru na wa haki, jambo ambalo anadaiwa hakulifanya na ameshinda uchaguzi kwa hila.

DK SLAA AMPASUA MBOWE HADHARANI – ASEMA CHADEMA INAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA -MBOWE VS LISSU

Leave A Reply