Marekani Yawashtaki viongozi wa Hamas kwa shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel
Marekani imemfungulia mashtaka Kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar na watu wengine kadhaa mashuhuri katika kundi hilo la Palestina kuhusiana na shambulio baya lililofanywa na Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana.
Wizara ya sheria imesema inawafungulia mashtaka wanachama sita wa Hamas kwa tuhuma saba, ikiwemo mauaji ya raia wa Marekani, kula njama za kufadhili ugaidi na matumizi ya silaha za maangamizi makubwa.
Malalamiko hayo ya jinai yanahusu miongo kadhaa ya madai ya mashambulizi ya Hamas, pamoja na shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa kusini mwa Israel karibu mwaka mmoja uliopita.
Ni hatua ya kwanza kwa vyombo vya sheria vya Marekani kuwawajibisha viongozi wa shambulio la Oktoba 7, ingawa watatu kati ya wale waliotajwa kwenye hati ya mashtaka wamekufa na Sinwar anaaminika kujificha kwenye vichuguu mahali fulani huko Gaza.
Katika taarifa yake ya video siku ya Jumanne, Garland alisema washtakiwa walihusika na kufadhili na kuongoza kampeni ya miongo kadhaa ya mauaji ya raia wa Marekani na kuhatarisha usalama wa Marekani”.