Marioo Atoa Onyo Kwa Mtu Anayetumia Jina Lake Kwenye Mtandao Wa X
![](https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2020/07/MARIOO.jpg)
Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayekimpiza kwa sasa na video ya Hakuna Matata, Marioo amesema kuwa hawahusiki na ukurasa wa Mtandao wa X (zamani Twitter) unaotumia jina la @tz_marioo ambao umekuwa unatumika kupotosha taarifa zisizo sahihi kutoka kwa msanii huyo.Marioo ameyasema hayo leo Julai 27, 2024 kupitia kwa mtaalamu wake wa mitandao ya kijamii ambaye pia ni IT wake, Michael Charles Chali.
“Ni kawaida kuwepo kwa matapeli katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha taarifa mbalimbali kwa ajili ya maslahi yao binafsi, hivyo uongozi wa mwanamziki wetu umeshachukua hatua kwa mtu anayetumia ukurasa huo na tunawaomba mashabiki wetu kupuuza taarifa zake ” amesema Michael Chali.