The House of Favourite Newspapers

Marubani Wazichapa Wakiendesha Ndege Angani, Habari Zasambaa Dunia Nzima

0

 

Ndege ya Shirika la Ndege la Air France

WAKIWA ndani ya chumba cha marubani wakiendesha ndege angani, marubani wawili wa Shirika la Ndege la Air France wanaripotiwa kuzichapa kavukavu.

 

Mtu ukiwa unasafiri kwa ndege, matukio kedekede yanaweza kutokea kwa upande wa abiria, lakini si tukio la kawaida kwa wale wanaotegemewa kuwafikisha salama –kwa maana ya marubani.

Tukio limeonekana kutokuwa la kawaida

Sasa; katika tukio lisilo la kawaida, mashirika ya habari ya kimataifa yameripoti kwamba marubani wawili walikorofishana na kurushiana ngumi huku safari ikiwa inaendelea angani.

 

Ngege hiyo ya Shirika la Ndege la Ufaransa ilikuwa inatoka Jiji la Geneva, Uswizi ikielekea jijini Paris, Ufaransa wakati tukio hilo lilitokea ndani ya chumba cha marubani kwa lugha ya kimombo cockpit.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zilichapishwa na vyombo vingi vya habari vya kimataifa, safari ya ndege iliendelea na kutua salama huku mzozo huo ukiwa haujaathiri safari iliyosalia, afisa mmoja alisema.

 

Gazeti la Uswizi la La Tribune liliripoti kwamba rubani na rubani msaidizi walizozana muda mfupi baada ya kupaa na kushikana mashati baada ya mmoja kumpiga mwenzake.

Marubani hao tayari wameshasimamishwa kazi

“Wafanyakazi wa cabin waliingilia kati na mfanyakazi mmoja aliongoza ndege katika chumba cha marubani,” ripoti ilisema.

 

Jarida la The Guardina la Uingereza liliripoti kwamba, habari za mapigano hayo ziliibuka baada ya shirika la uchunguzi wa anga la Ufaransa la BEA kutoa ripoti wiki iliyopita ikisema kwamba baadhi ya marubani wa Air France wana kosa nidhamu katika kuheshimu taratibu wakati wa matukio ya usalama.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply