The House of Favourite Newspapers

Marufuku Kusafirisha Mtoto Chini ya Miaka 18 Bila Kibali

0

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, ameviagiza vyombo vya Ulinzi na Usalama kuhakikisha kila mtoto mwenye miaka chini ya 18, anayesafirishwa kutoka eneo moja kwenda jingine anakuwa na kibali cha mzazi na cha kiongozi wa Serikali za Mitaa.

 

Katika maadhimisho ya siku ya kupinga biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, amebainisha kuwa Wizara itajikita kusimamia safari za ndani ya nchi kwa lengo la kubaini wanaojihusisha na vitendo hivyo.

 

Waziri huyo amesema waathirika wakubwa wa biashara ya binadamu ni Wanawake na Watoto na wengi hujikuta kwenye vitendo hivyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo tamaa ya pesa na kuibuka kwa soko la vitendo vya ngono.

 

Inakadiriwa kwa mwaka Duniani kote, asilimia 72 ya waathirika wa biashara haramu ya binadamu ni wanawake na mabinti ambao wengi hutumiwa kwenye vitendo vya ngono na udhalilishaji wa kijinsia.

 

Leave A Reply