The House of Favourite Newspapers
gunners X

Massanza: Habibu Kyombo Aliomba Kuvunja Mkataba na Taratibu Zote Zilizingatiwa

0
Hussein Masanza Meneja wa Habari na Mawasiliano Singida Big Stars

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Singida Big Stars iliyo na maskani yake mkoani Singida Hussein Massanza amesema kuwa mchezaji aliyesajiliwa na klabu hiyo kutoka klabu ya Mbeya Kwanza iliyoshuka daraja Habibu Kyombo ameiomba klabu hiyo kuvunja Mkataba kutokana na kuwa na malengo makubwa Zaidi.

 

Meneja huyo amebainisha kuwa Kyombo alitoa sababu amabzo kimsingi mwanzo zilikuwa ni ngumu kwa klabu kukubaliana naye lakini baadaye waliangalia maslahi mapana ya klabu namchezaji ambapo hekima ilitumika na mkataba ukavunjwa rasmi.

Masanza amebainisha kuwa malengo ya Singida Big Stars kwa msimu ujao ni kumaliza katika nafasi nne za mwanzo (Top Four) kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC

Amesisitiza pia kuwa Menejimenti ya Habibu Kyombo ilitekeleza taratibu zote zinazotakiwa kufanyika ili kuvunja mkataba na kwa kufanya hivyo pande zote mbili zilikubaliana na hatimaye kama klabu kumtakia Kyombo mkono wa kwaheri.

Habibu Kyombo alisajiliwa na Singida Big Stars kabla ya kuvunja mkataba wake na Klabu hiyo

Aidha amesisitiza kuwa Kyombo wakati anasajiliwa halikuwa pendekezo la kocha bali ni Kamati ya Usajili ya Klabu hiyo ndiyo ilimsajili kwa kuangalia sifa zinazofanana na zile za mapendekezo ya Kocha.

 

Kwa upande mwingine Meneja huyo wa Habari na Mawasiliano amebainisha kuwa Singida Big Stars inafanya usajili wa kuhakikisha msimu ujao inaingia katika mbio za Ligi Kuu kusaka nafasi nne za juu ikiwa na lengo la kushiriki katika mashindano ya kimataifa.

Leave A Reply