The House of Favourite Newspapers

Masauni Aagiza Trafiki Waliomshambulia Dereva na Abiria Wawajibishwe

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameonesha kukerwa na kitendo cha askari wa wawili wa Kikosi cha Usalama Barabarani, ambao wameonekana kwenye video kupitia mitandao ya kijamii wakimtukana dereva na kumpiga yeye na abiria wake huku akieleza kuwa tayari wamekamatwa na kuwekwa ndani ili sheria ichukue mkondo wake.

 

Kukamatwa kwa askari hao kumetokana na agizo lililotolewa na Mhandisi Masauni ambapo amesema katu Serikali haiko tayari kuona Jeshi la Polisi likichafuliwa na baadhi ya askari waliokosa uadilifu.

Akizungumza leo ijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya uchoraji la usalama barabarani, Masauni amesema kumekuwa na malalamiko mengi ya madereva kubambikiwa makosa au askari kufanya vitendo vilivyo kinyume na mwenendo mwema wa jeshi la polisi.

 

“Kuna video ambayo tangu jana imeonekana ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonesha askari wakimtukana dereva pamoja na abiria waliokuwamo na si hivyo tu ilifika hadi kumpiga. Baada ya tukio hili nilimuagiza Kamanda wa Kiko cha Usalama Barabarani achukue hatua kwa suala hili. Kwa taarifa ambazo ninazo tayari wamekamatwa,”amesema.

 

Amesema ikitokea mtumiaji yoyote wa barabara amefanyiwa vitendo vyovyote asisite kuwasiliana na uongozi wa askari aliyefanya vitendo hivyo.“Na ikitokezea uongozi wa askari husika anatetea au kutochukua hatua muafaka, mlalamikaji apande kwa uongozi wa juu na ikibidi afike hata kwangu nani mitachukua hatua stahiki na utapata mrejesho.

 

Kuhusu suala la usalama barabarani, Mhandisi Masauni amesema anaipongeza Kampuni ya Mafuta ya Puma kwa kuendesha program hiyo ambapo pia alizitaka kampuni zingine kuiga mfano huo kwa kuwekeza kwenye ulinzi na usalama wa watoto kwani ni Taifa leo kesho na wateja wa kesho pia.

 

“Programu hizo zimekuwa zikikabiliw na changamoto mbalimbali za kifedha. Ninaomba kutumia fursa hii kuomba uongozi wa Puma kukisaidia Kikosi cha Usalama Barabarani kuzifikia shule zote nchini kwa kupitia askati walioko kwenye maeneo yote nchini.

 

“Namuagiza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani kuanza mchakato wa kuandaa andiko la kutoa mafunzo kwa shule zote nchini na kuliwasilisha kwenu (Puma) ili muone namna yambavyo mnaweza kusaidia kuokoa kizazi chetu cha kesho,” alisema Masauni.

 

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa Puma Energy Tanzania Ltd, Dominic Dhanah amesema kwa mwaka huu programu hiyo itafanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar na kuzihusisha zaidi ya shule 16.

 

“Tumefanya utafiti na kugundua katika shule tulizoendesha, baada ya mafunzo haya ajali kwa wanafunzi zimepungua ndio sababu tumeamua kuongeza idadi ya shule,” amesema Dhanah.

ROUND ABOUT: Mwahangila auza gari kufanya promo/Nguvu ya kitambaa madhabahuni

Comments are closed.