Masele Aunganisha Nguvu na Katambi Shinyanga Mjini

MGOMBEA Ubunge wa jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi, jana Jumanne Agosti 25, 2020 amerudisha fomu Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ya kuomba kugombea ubunge kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo hilo, Geofrey Mwangulumbi, huku aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Stephen Masele, akimuahidi kushirikiana naye bega kwa bega katika kukiletea ushindi CCM.

 

 

Katambi alikuwa ameambatana na viongozi na wanachama wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakari Gulam na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Stephen Masele, ambaye ameahidi kufanya kampeni kwa amani na utulivu.

 

 

Masele ameahidi kupigana kufa na kupona kuhakikisha CCM inashinda ngazi zote za udiwani, ubunge na rais katika Jimbo la Shinyanga Mjini.

 

 

Aidha Masele amewataka Wana-CCM kuungana na kuwaomba kuvunja makundi yaliyokuwepo na badala yake kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa na chama huku akisisitiza kuwa atakuwa bega kwa bega na Katambi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa 2020.

 

 


Toa comment