Masele Awekwa ‘Mtu Kati’ Kamati ya Maadili Bunge

MBUNGE wa Shinyanga Mjini (CCM) na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament – PAP), Stephen Masele amefika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge jijini Dodoma kujibu tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili.

Amefika mbele ya Kamati hiyo leo Jumatatu, Mei 20, 2019 kuitikiaw ito wa Spika wa Bunge, Job Ndugai,  aliyemtaka kufika leo ili ajibu tuhuma zinazomkabili.

Masele hivi karibuni aliingia kwenye mgogoro mzito na Rais wa PAP, Roger Nkodo Dang,  nchini Afrika Kusini ambaye anatuhumiwa kuwadhalilisha wanawake, hivyo Masele akamkomalia apishe nafasi hiyo kwa ajili ya kuchunguzwa na Umoja wa Mataifa, lakini aligoma.

Jambo hilo linadaiwa kusababisha mgogoro mkubwa miongoni mwa viongozi hao wawili, hivyo Ndugai akamtaka arejee nchini.

 

Tutaendela kukujuza kitakachojiri baada ya Masele kuhojiwa leo.

 

TAZAMA MASELE AKIWASILI BUNGENI LEO


Toa comment