Masele Chapombe Azawadiwa Mtaa

Masele na Mkewe.

STORI: GABRIEL NG’OSHA | RISASI | MIKITO NUSUNUSU

WAKAZI wa Goba jijini Dar, wamemzawadia  Mchekeshaji, Cypriane Masele kwa kuuita mtaa wao jina la Masele Street  kutokana na kuikubali kazi yake ya uchekeshaji.

Masele alifunguka hayo hivi karibuni alipokuwa akipiga stori mbili tatu na Mikito Nusunusu ambapo alisema kwa kutambua thamani ya jina lake kwenye sanaa, wakazi wa Goba wamempa hiyo heshima kwani wanampenda na ndiyo maana wameamua kuupa mtaa jina lake.

“Ni upendo wa dhati sana waliouonesha wakazi wa Goba kwa kuuita mtaa wao jina langu la Masele Street, ninawathamini na kuwaheshimu kama walivyoniheshimu wao, si kitu kidogo mtaa kuitwa jina lako ni thamani kubwa sana,” alisema Masele.

Wiki Moja Baada ya Ndoa, Masele Chapombe Amtongoza Upya Mke Wake

Save

Save

Save

Save


Toa comment