The House of Favourite Newspapers

Mashabiki wa Japan Wasafisha Uwanja Baada ya Kuishinda Ujerumani Kombe la Dunia

0

MASHABIKI wa timu ya Japan Novemba 23, 2022 wamewashangaza wengi baada ya kuanza kuokota taka uwanjani mara baada ya mchezo wao dhidi ya Ujerumani kumalizika.

Japan wamepata ushindi wa 2-1 dhidi ya mabingwa hao mara nne katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia,  walisitisha sherehe kwa muda katika Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa nchini Qatar ili kuusafisha kwanza.

Unaweza kusema walifanya hivyo kwa madhumuni ya kuonekana, lakini itakumbukwa walifanya hivyo pia mwaka 2018 katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Walipoulizwa kwanini wanafanya hivyo, mmoja wa raia wa Japan alisema hawana utamaduni wa kuacha taka nyuma.

Leave A Reply