The House of Favourite Newspapers

Mashabiki Wa Soka Walonga na Championi

0

 

Mashabiki wa timu ya Yanga.

SHAMBA jipya nyani walewale kwa hiyo sioni kipya Msimbazi Okwi sanamu la Simba, Niyonzima kama anaweza akacheze nje, big up Msuva kazi njema.Wasiliana  255 654 941010 Facebook: championigazeti Twitter:
championinewspaper E_mail: [email protected]

Fadhiri Dady, Malengo Kilwa.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

THIS is Simba huku Kichuya kule Okwi katikati Bocco nyuma Niyonzima mbona watakoma.

Hamisi Sabahi, Vingunguti Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

KWA kweli Simba hii hadi raha, tunajua yebo kilichowakosti ni ukata hamjapenda kuwa hivyo, mtatusamehe tarehe 23 hapa Okwi, Kichuya pale Bocco, ahaaa kumbe hampendi au!

Saadati B. H Tanga.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

KWA kiki, hii mitambo ya Simba inafanya kazi hatoki mtu, Manula golini, Bocco kama kawaida pamoja na Kichuya halafu kuna nahodha Mwanjali, hadi rahaa.

Michael Tomas Richard, Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

YANGA raha sana siyo hao Simba wanalilia ubingwa watasubiri sana tu.

Sundy Kibanda, Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

YANGA daima mbele nyuma mwiko, ni mwendo wa ushindi mwanzo mwisho mpaka kieleweke.

Raphael Kigodi, Iyunga Mbeya.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

TFF mwaka huu msitupangulie ratiba ya ligi kuu kama haitapanguliwa basi mzunguko wa kwanza Simba haitapoteza mchezo hata mmoja, penalti 45, tutachukua ubingwa bila wasiwasi, mwenye mzigo aweke.

Miraji Chamke, Tandai Kinore.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

CHAMA langu Simba msijiamini sana, fanyeni mazoezi ya nguvu ili tarehe 23 tuwamalize mapema wale jamaa zetu. Simba nguvu moja.

Osward Mlangwa, Magomeni DSM.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

KWA Simba hii mjipange, treni limekatika breki atakayekatiza halali yetu.

Abuu Lukindo, Kimara Bonywoka.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

OMOG, Bocco na Okwi mfumo hauendani wachezeshe Okwi na Mavugo uone mabao yanavyoingia.

Joseph Gicha, Mto wa Mbu.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

SALAMU zangu kwa watani wangu Yanga, kaja Okwi wa 5-0 tukutane tarehe 23.

Ombeni Mwankemwa, Kyela Mbeya.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

YANGA ndiyo timu kubwa na maneno ya mtani wangu Simba hata kwenye kanga yapo, kubwa tulia unyonyolewe tarehe 23.

Lilungulu Yusto, Nachingwea.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

YANGA kwa mechi ya magazetini daah! Wanasimba mmetushinda sasa hebu tusubiri hiyo tarehe 23 hapo TMK.

Gasper Komba a.k.a Kahamuhamu safarini Zambia.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

YANGA mdogomdogo hatuogopi zogo kwa watoto wadogo ndiyo maana tumekuja kama mbogo sikilizeni kichapo tarehe 23.

Adam Magong’o, Makuyuni Korogwe Tanga.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

HONGERENI Simba kwa usajili mlioufanya, nawapongeza viongozi kwa ushirikiano wenu nyie wazee kaeni kando waacheni viongozi wafanye yao migogoro hatuitaki.

Ramadhani Modeli, Soko la Uzunguni Mkwakwani Tanga.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

NYIE mikia tutawanyoosha kama tulivyowanyoosha mlivyotoka Brazil mwaka 1983.

Hamisi Digila, Kibaha Kongowe.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

YANGA mnachonga sana kumbukeni Agosti 23 siyo mbali kwa nguvu za Mungu tutawafunga 3-0 ndiyo mjue Simba ya mwaka huu moto.

Mchibuyu Bakari Supaki, Mtoni.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

KWA usajili huu uliofanywa na Yanga, sijui Simba kwenye Ngao ya Jamii watatokea mlango gani.

Ibrahimu Dikwanga, Mbezi Luis Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

KWA Simba hii mtafungwa sana tu kwani kila idara imekamilika mwanzo mwisho, nyuma kati mbele we acha tu.

Edwin Coelho, Changombe Dodoma.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

HIVI lini Simba ilikuwa mbovu? Maana naona mashabiki wao mitaani wamepagawa na timu yao utadhani tayari wameshabeba ubingwa, waangalie sana.

Kennedy Mwailolo, Mbeya.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

SINGIDA United leteni jezi tununue.

Bosi Mwanga, Singida Mjini.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

MNYAMA unyamani Agosti 23, jamani kwa mziki wa mnyama Simba kwa sasa hiyo Agosti 23 mtumbuizaji si mwingine bali ni mama wa majanga Snura na songi lake la taifa la kucheza kichura chura, ‘so’ hao Vyura FC wajipange kuja kunengua kivyura vyura.

Swaibu R. Lambanyonge, Kilimanjaro.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

NAONA mzee Okwi amerudi, kuwatesa wazee wenzake Cannavaro na Yondani, tukutane kwa Mchina Agosti 23, Okwiiii.

Mikidadi Rashid, Vingunguti kwa Simba, Dar.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

CHAMPIONI buaana! Hivi tumeona wapi chura juu ya mti au kapandishwa? Kampa kampa tena bado inawasubiri.

Pancho wa Mirerani.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

YANGA raha sana naomba tuzidishe ukimya ili siku ya mechi tuwaaibishe hao wa matopeni maana wanachonga sana.

Godwin Ngonela, Moshi.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••

NAITAKIA timu yangu ya Simba maandalizi mema kwenye pambano lao la Ngao ya Jamii.

Nadili J Masami, Musoma Mara.

  • ••••••••••••••••••••••••••••••••••
  • 255 654 941010 Facebook: championigazeti Twitter:
    championinewspaper E_mail: [email protected]
Leave A Reply