The House of Favourite Newspapers

Mashabiki wa Timu ya Taifa ya Brazil Waitelekeza Jezi ya Njano Kisa Inafanana na Bendera ya Chama Tawala

0
Mashabiki wa timu ya taifa ya Brazil

MASHABIKI wa timu ya taifa ya Brazil wamepunguza mapenzi yao ya kuvaa jezi ya njano ya timu hiyo kisa chama tawala cha Rais aliyepo madarakani kwa sasa kinatumia rangi na bendera ya timu hiyo kama mtaji wa kisiasa kwa kuzigeuza kuwa rangi za bendera za chama hicho.

 

Utafiti umefanyika ikiwa zimebaki siku 54 hadi kuanza kwa mashindano ya Kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini Qatar ambapo imebainika kuwa licha ya kuwa jezi ya njano ya timu hiyo imekuwa ikiheshimika na kuhesabiwa kama alama ya bahati, ushindi na mafanikio ya raia wa nchi hiyo lakini imekuwa ikitumika kinyume na maslahi ya raia wengi ambao wana mitazamo tofauti ya kisiasa.

 

“Kuvaa jezi ya njano ilikuwa kama alama ya heshima, ni alama ya ushindi kwangu. Nilikuwa nikiivaa siyo tu kwenye mechi za timu ya taifa lakini pia katika majukumu yangu ya kila siku, kwa sasa nimeacha kuivaa kutokana na sababu za kisiasa. Rais wa sasa pamoja na wapambe wake wameibadilisha jezi ya timu ya taifa kama sehemu ya kampeni za kisiasa na alama ya chama chake cha siasa.” alisema shabiki mmoja wa timu ya taifa ya Brazil.

Neymar Jr akiwa amevaa jezi ya blue ya timu ya taifa ya Brazil

Shabiki huyo aliendelea kueleza kuwa hawezi tena kuitundika jezi hiyo katika viunga vya nyumba yake kwani hataki kutafsiriwa tofauti na wenzake kutokana na kutounga mkono sera za chama hicho cha siasa.

 

Jezin ya njano ya timu ya taifa ya Brazil imekuwa ikijulikana kwa jina maarufu la Canarinho na siyo jezi pekee ya timu hiyo ya taifa kwani zipo jezi nyingine zenye rangi tofauti kama bluu pamoja na nyeupe.

 

Timu ya Taifa ya Brazil inatarajiwa kutoa upinzani mkali katika mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika nchini Qatar mwishoni mwa mwaka huu.

Leave A Reply