The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mashabiki wa Vemoney Wamshambulia Bella, Kisa Jux

BAADA ya hivi karibuni msanii wa Bongo Fleva, Isabella Mpanda ‘Bella’ kuposti picha yake akiwa na msanii mwenzake, Juma Khalid ’Jux’ kwenye ukurasa wake wa Instagram kisha kusindikiza na maneno yaliyoashiria yupo kwenye uhusiano naye wa kimapenzi, mashabiki wamemnanga kuwa asijisumbue kwani haendani na jamaa huyo.

 

Bella aliandika hivi katika ukurasa wake; “Nyie timu Vanessa mnikome huyo bosi wenu ana viuno vya Kimakondee? Pumbavu zenu, niacheni nipone, mimi naitwa pipi ya Kusini.”

 

Alimaliza kwa kuandika hivyo ndipo mashabiki wa Vanessa (aliyekuwa mpenzi wa Jux) kwa hasira wakaanza kumshushia matusi kuwa anajihangaisha tu, Jux hawezi akatembea na msichana wa dizaini yake.

 

“Hasa atajiringanisha na Vee (Vanessa)! Vee kamzidi kila kitu, kuanzia pesa mpaka dhambi,” aliandika Hilda Helly.

 

“Jux hawezi akatoka na mwanamke mchafu kama wewe, unajihangaisha tu wala hamuendani, kwanza akupeleke wapi? Embu tuondolee uchuro wako hapa, Jux anatembea na watu wanaojielewa ndiyo maana akamchagua Vanessa,” alikomenti Hapyxlucas shabiki toka Insta.

Comments are closed.