Mashabiki wa soka leo wameendelea kujazana nje ya ofisi za Shirikikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kusubiria hatima ya aliyekuwa mchezaji wa Yanga Benard Morisson aliyeukana mkataba wa kuichezea timu hiyo miaka miwili.
Akiwa ameukana mkataba huo amedaiwa kusaini kwa kuchezea mahasimu wao Simba mkataba wa miaka miwili.
Kesi hiyo ambayo ilitarajiwa kutolewa uamuzi juzi (Jumatatu) imeendelea kuleta mvutano wa hoja kutoka upande wa mchezaji huyo na Yanga hivyo kusababisha umati wa mashabiki hao kujazana nje ya ofisi hizo kwa siku tatu mfululizo sasa.
Umati huo umesababisha wanausalama nao kupiga kambi eneo hilo ambapo mwandishi wetu alishuhudia askari wa difenda, pikipiki na askari kanzu waliokuwa wakiimarisha doria eneo hilo.
Mashabiki walijazana nje ya ofisi hizo wasikika kubishana kundi moja likiwa upande wa mchezaji huo na upande mwingine upande wa Yanga.