The House of Favourite Newspapers

Mashabiki Walivyomvamia DIAMOND Hotelini Mwanza – Video

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, na crew nzima ya wasanii watakaopafomu leo kwenye Tamasha la Wasafi Festival wamewasili jana katika Uwanja wa Ndege jijini Mwanza uliyopo Ilemela mkoani humo.

Baada ya kutua Mwanza, Diamond na wenzake wakaeleka katika hoteli waliyopangiwa kufikia lakini mashabiki hawakubaki nyuma matokeo yake wakamsindikiza mpaka hotelini hapo hali iliyozua tafrani na kusababisha walinzi kuingia kazini kuwasambaratisha mashabiki hao.

Tamasha la Wasafi Festival mkoani Mwanza linatarajiwa kufanyika leo Jumamosi ya Desemba 15, katika Uwanja wa CCM Kirumba, ambapo steji itashambuliwa na wasanii kibao akiwemo Diamond, Rayvanny, Harmonize, Mbosso, Young Killer, Gigy Money. Temba, Dulla Makabila, Dudu Baya na wasanii wengine.

 

 

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO ZIMA 

Comments are closed.