The House of Favourite Newspapers

Mashabiki ‘wamteka’ mwamuzi mechi ikiendelea

0

ndondo

Mohammed Mdose, Dar es Salaam

MASHABIKI wa timu ya Friends Rangers, jana Jumanne uvumilivu uliwashinda baada ya kuchukua maamuzi magumu ya ‘kumteka’ mwamuzi wa pembeni aliyekuwa akichezesha mchezo wao dhidi ya Misosi FC kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni, Dar.

Mchezo huo wa hatua ya 32 Bora ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup, ulimalizika kwa Misosi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Idd Selemani dakika ya 31.

Championi lililokuwepo uwanjani hapo, liliwashuhudia mashabiki hao dakika ya 80 wakimbeba mwamuzi huyo ambaye jina lake halikufahamika haraka kwa madai kuwa alikuwa akiionea timu yao.

Hata hivyo, mwamuzi huyo aliachiliwa na kurudi uwanjani kumalizia mchezo huo ambao muda mwingi ulitawaliwa na vurugu zilizokuwa zikifanywa na mashabiki wa Friends.

Leave A Reply