The House of Favourite Newspapers

Mashambulio ya Urusi Yasababisha Kukatika kwa Umeme Ukraine

0
Shambulio la Ukraine dhidi ya Urusi

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa mashambulio yanayofanywa na Urusi yanalenga maeneo muhimu yanayozalisha  umeme hali inayosababisha kukosekana kwa nishati hiyo muhimu.

Kutokupatikana kwa umeme Ukraine kumesababisha  takribani mamilioni ya wakazi wa nchi hiyo kuathirika  kwa nishati hiyo.

                                     Shambulio la Urusi kukata umeme Ukraine

Meya wa Kharkiv Ihor Terekhov alisema mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundombinu ya raia yaliacha sehemu kubwa ya jiji lake bila umeme na maji Jumapili jioni. Aliliita jaribio hilo baya na la kijinga la kulipiza kisasi.

Terekhov na Gavana wa eneo hilo walitoa wito wa utulivu, wakisema huduma za dharura zinafanya kazi ya kurekebisha uharibifu na kuzima moto.

Imeandikwa: Leocardia Charles kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply