The House of Favourite Newspapers

Masharti Mapya ya WhatsApp Kuanza kesho

0

WhatsApp imetaja Jumamosi ijayo kuwa siku ya mwisho kwa mamilioni ya wateja wake kukubali masharti mapya ya utumiaji wa mtandao huo ambao ulikosolewa sana katika mitandao ya kijamii huo mwanzoni mwa mwaka huu.

 

Kupitia masharti hayo mapya, mtandao huo unawataka wateja wake isipokuwa wale wanaoishi Ulaya kukubali kugawa data yao na facebook, kampuni kuu ya mtandao huo wa kutuma ujumbe. Kuanzia Ijumaa hii , wale ambao hawatakubali masharti hayo wataanza kupata hudumu chache.

 

”Hakuna akaunti ya mteja itakayofutwa ama mtandao huo kuondolewa kwa mteja ifikiapo tarehe 15 Mei” , ulisema mtandao huo katika tovuti yake.

 

Lakini ni yapi yatakayotokea iwapo utakataa kukubali masharti hayo mapya?

Kushindwa kuona taarifa

Kufikia tarehe 15 mwezi Mei, wale ambao hawatakubali masharti mapya hawataweza kuona orodha ya watu waliotumia na ujumbe nao wanapofungua huduma hiyo. Lakini unaweza kujibu simu na simu za video.

 

”Iwapo mfumo wako wa taarifa unafanya kazi , unaweza kugusa ili kuzisoma ama kujibu ujumbe mbali na kujibu simu ulizokosa au simu za video”, inasema kampuni hiyo.

 

Wateja hao wataweza kuwasiliana na wanaowasiliana nao kupitia taarifa zinazojitokeza katika skrini iliyowashwa. Iwapo baada ya wiki chache , watumiaji bado hawatakubali masharti hayo hawatoweza kupokea simu ama arifa na kwamba mtandao wa WhatsApp utasita kutuma jumbe na simu kwa simu zao.”

 

”Vikwazo hivyo havitawaathiri watumiaji kwa wakati mmoja”, kampuni hiyo imesema.

Ujumbe wa kukukumbusha

WhatsApp inasema kwamba katika wiki za hivi karibuni imekuwa ikiwatumia wateja wake taarifa ili kukubali masharti hayo, iwapo hawajakubali.

 

Imesisitiza kuwa katika siku chache zijazo , ujumbe huo wa kuwakumbusha wateja utaonekana mara kwa mara hadi pale watumiaji wa mtandao huo watakapofikia uamuzi.

 

Ijapokuwa mtandao huo hautafuata akaunti za wale ambao hawatakubali masharti hayo mapya , WhatsApp itatumia sera yake dhidi ya akaunti ambazo hazifanya kazi.

 

”Masharti haya yanasema kwamba iwapo mteja hajatumia mtandao kwa siku 120 , akaunti hiyo itafutwa ili kuimarisha usalama , kupunguza uhifadhi wa data na kulinda faragha ya watumiaji.”

 

Wateja wanaweza kuhamisha historia ya chati zao kama hatua mbadala ya wao kutopoteza mawasiliano yao.

 

Masharti mapya yaliozua utata

Mapema mwaka huu , WhatsApp ilitangaza mabadiliko kuhusu masharti ya huduma yake.

 

Ilisema kwamba baadhi ya data yake kutoka kwa wateja wake kama zile za mawasiliano na maelezo mafupi zitagawiwa kampuni ya facebook na kwamba pia itaweza kufanya hivyo hivyo na mitandao ya Instagram na Messenger.

 

Watumiaji kutoka Muungano wa Ulaya na Uingereza , ijapokuwa ni sharti wakubali masharti mapya mabadiliko hayo hayatakuwepo katika akaunti zao. Masharti hayo mapya yalizua wimbi la maswali kuhusu masharti ya faragha.

 

Baadhi ya watumaiji walianza kutafuta mbadala wa WhatsApp kama vile Telegram au Signal. Ni kutokana na ukosoaji kama huo WhatsApp iliamua kuahirisha siku ya mwisho ya masharti hayo hadi Mei 15 ili kufafanua uvumi na habari za uongo kuhusu swala hilo.

 

”Tunataka kufafanua kwamba masharti hayo mapya kuhusu sera hiyo hayaathiri kwa njia yoyote faragha ya ujumbe ambao wateja husambaziana na marafiki zao au familia”, ilisema kampuni hiyo.

 

WhatsApp na facebook hazina uwezo wa kusoma ujumbe wako au kusikiliza mawasiliano yako ya simu na marafiki , watu wa familia ama wafanyakazi wenzako waliopo katika WhatsApp. Kila kitu unachosambaza kitasalia kati yako, mtandao huo ulisema katika taarifa yake siku ya Jumatatu.

Leave A Reply