The House of Favourite Newspapers

Mashetani Wameamka, Ubingwa Unanukia

0

 MWAKA mpya wa 2021 ni leo, ndiyo kwanza umeanza na bahati nzuri kwa mashabiki wa Manchester United ni kuwa timu yao inauanza mwaka huu ikiwa moja ya timu zinazowania ubingwa wa Premier League.

 

United inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa nyuma ya Liverpool na kama leo itashinda mchezo wake dhidi ya Aston Villa basi itakuwa pointi sawa na Liverpool.

 

Wakati msimu huu ukianza, hatua za mwanzo pekee zilitosha kuitoa United katika mbio za ubingwa na kuonekana wanaweza kukosa hata kuingia katika nafasi nne za juu, lakini ghafla upepo umebadilika na sasa timu hiyo inatajwa kuwa moja ya zinazowania ubingwa.

Maamuzi ya viongozi wa United kuamua kuendelea kumvumilia kocha wao, Ole Gunnar Solskjaer inawezekana yamechangia kuibadilisha timu hiyo na sasa imewashangaza wengi kwa kushindana pointi na Liverpool licha ya kuwa miezi kadhaa nyuma United ilichapwa mabao 6-1 na Tottenham.

 

Kuna mambo kadhaa ambayo yametajwa kuwa ni sababu ya upepo kubadilika na United maarufu kwa jina la ‘Mashetani Wekundu’ kuingizwa katika timu zinazowania ubingwa, nazo ni hizi:

 

UBORA WA BRUNOTangu aliposajiliwa Januari, mwaka jana, Bruno Fernandes amekuwa staa mkubwa na kusaidia hata wenzake kucheza kwa ubora wa juu.

 

WASHAMBULIAJI WAKALI

Wakipewa nguvu na Fernandes nyuma yao, kumekuwa na uchu wa mabao kutoka kwa Marcus Rashford, Anthony Martial, Mason Greenwood na Edinson Cavani.

 

MABEKI KUPUNGUZA MAKOSA

Moja ya makosa makubwa yaliyoiangusha United kipindi cha nyuma ni makosa ya walinzi, lakini sasa wameimarika na makosa yanapungua.

 

HAKUNA KUKATA TAMAAIle kauli mbiu yao ya ‘NEVER-SAY-DIE’ ni kama imerejea na sasa hawakati tamaa hata kama wakianza kufungwa, wao hadi filimbi ya mwisho ndiyo wanakubali matokeo.

Leave A Reply