The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mashindano Ya Kuran Yaahirishwa jijini Dar

0
Mwenyekiti wa maandalizi ya kamati ya mashindano hayo, Shehe Nuurdin Kishki kutoka taasisi ya Al-Hikma.

Kamati ya maandalizi ya mashindano maalum ya kusoma kuran Afrika yaliyotakiwa kufanyika jijini Dar Mei 10 mwaka huu imeyasitisha mashindano hayo kisa corona.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo Mwenyekiti wa maandalizi ya kamati ya mashindano hayo, Shehe Nuurdin Kishki kutoka taasisi ya Al-Hikma amewaomba radhi wadau wote waliokuwa wakitasubiri kwa hamu mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kwa mafanikio makubwa hapa nchini.

 

Hata hivyo shehe huyo amesema mashindano hayo yatafanyika siku nyingine ambayo itapangwa baada ya hali ya maambukizi ya virusi vya corona itakapokuwa nzuri na serikali kuondoa kuzuizi cha mikusanyiko.

Shehe Kishki amesema maandalizi yote ya mashindano hayo yalikuwa tayari kwa asilimia 95 lakini mambo yamekwenda isivyotarajiwa.

 

“Maandalizi ya mashindano hayo yalikuwa yameshakamilika kwa asilimia 95 lakini ugonjwa wa Covid-19 umetuharibia.

 

Mwaka huu nchi 20 zilikuwa zimeshathibitisha kushiriki mashindano hayo ambapo hata mwaka jana pia yalifanyika Uwanja wa Taifa Dar ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

HABARI: NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL  

Leave A Reply