Mashindano ya Utamaduni ya Mkuu wa Majeshi Yalivyohitimishwa na Washindi Kupatiwa Zawadi
Dar es Salaam 30 Agosti 2024: Mashindano ya Utamaduni ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jacob John Mkunda yaliyokuwa yakirindima kwenye Ufukwe wa Msasani Club jijini Dar kuanzia Agosti 19 mwaka huu, jana yalihitimishwa rasmi na washindi kujitwalia zawadi mbalimbali.
Mashindano hayo yalihusisha vikundi vya ngoma za utamaduni na bendi za muziki wa dansi jumla makundi 19 kutoka Jeshi la Wananchi (JWTZ) mikoa mbalimbali.
Katika tukio hilo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Stergomena Tax aliyekuwa na Naibu Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu kama MwanaFA sambamba na mwenyeji wa mashindano hayo, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob John Mkunda.
Akizungumza na Wanahabari Mkuu wa Majeshi alisema pamoja na mambo mengine lengo la mashindano hayo pamoja na kufufua sanaa za utamaduni zilizokuwa zimefifia tofauti na ilivyokuwa zamani na kubwa zaidi ni shamrashamra za kuelekea miaka 60 ya JWTZ. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN/GPL