The House of Favourite Newspapers

Mashine Mpya Yanga Yapania Rekodi

0

SAIDO Ntibanzokiza, ingizo jipya ndani ya Klabu ya Yanga akitokea nchini Burundi kwa kusaini dili la miaka miwili, amesema kuwa atashirikiana na wachezaji wenzake ili kufanya vizuri zaidi.

 

Akiwa amecheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara baada ya kusaini dili hilo akiwa ni mchezaji huru ila akifanya mazoezi na Klabu ya Vital’O ya Burundi, amehusika kwenye mabao manne kati ya 28 yaliyofungwa na Yanga.

 

Amefunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.  Mchezo wake wa kwanza ulikuwa ni dhidi ya Dodoma Jiji ambapo alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

 

Mchezo wake wa pili ulikuwa ni dhidi ya Ihefu FC ambapo alitoa jumla ya pasi mbili za mabao Uwanja wa Sokoine, Mbeya. Nyota huyo amesema kuwa atashirikiana na wachezaji wenzake kuendelea kufanya vizuri.

 

“Bado kuna kazi ya kufanya ndani ya Yanga, ninaamini kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu inapata matokeo, nami nitafanya hivyo. Kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu ninaamini kwamba tutafanya vizuri hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,” aliongeza.

 

Leave A Reply