Masista Wanne wa Kanisa la Katoliki Watekwa Nyara na Watu Wasiojulikana
MASISTA wanne wa kanisa la Katoliki wametekwa nyara na watu wasiojulikana katika Jimbo la Imo lililopo Kusini Mashariki mwa Nigeria.
Polisi wa Nigeria wametoa taarifa hiyo na kueleza kuwa hali hiyo imeshamiri nchini humo na lengo kuu ni kwa ajili ya kupata fedha kama fidia ya kuwaachia.
Msemaji wa Polisi wa Imo, Michael Abattam amesema kuwa masista hao walitekwa Agosti 21, 2022 karibu na Mji wa Okigwe, wakati wakiwa njiani kuelekea kwenye misa.
Abbatam ameeleza kuwa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo ambapo kwa sasa linachukuliwa ni jambo la kawaida katika nchi hiyo.
Ripoti inaeleza kuwa nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi mara kwa mara na kuandamwa na uhalifu.
Mara nyingi wahalifu huwateka viongozi wa dini siyo kwa sababu za kidini au kiitikadi, bali ni kwa sababu kanisa hilo linanaloonekana kuwa na uwezo wa kuhamasisha waumini kulipa fidia kwa ajili ya kuwaokoa watu waliotekwa nyara.
Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao