Maskini Mbosso: Aanika Siri Nzito na Marehemu Martha

MSANII wa Bongo Fleva kutoka Lebo ya WCB, Mbosso, ameamua kuweka wazi siri ya muda mrefu iliyokuwepo kati yake na marehemu Martha ambaye ni msanii wa vichekesho aliyefariki mapema wiki hii.

 

Akionekana kuguswa  na msiba huo, Mbosso ameweka wazi kuwa yeye na Martha hawakutaka kuweka wazi kwa watu kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu (zaidi ya miaka mitano), na kuwa walikuwa na mtoto waliyezaa pamoja.

Mbosso amemwombea marehemu pumziko jema kwa Mwenyezi Mungu na kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kuwa –

“Licha ya Vipingamizi Vingi juu ya Mimi kuwa na Wewe takribani au ndani ya zaidi ya Miaka Mitano (5) iliyopita, hatukuacha kuonyeshana ni kiasi gani tulikuwa tunahitajiana sana kwenye Safari yetu ya maisha.

“Japo jitihada zetu hazikuweza kufanikisha Mimi na wewe Kuwa Pamoja .., ila mbegu tuliyoipanda vuno letu ulichagua Liwe siri baina yangu Mimi na wewe.., sikukubishia japo Mwazoni nilikukatalia kwa sababu ‘najijua kifua cha Kuficha Siri sina..’ , ila nikakuahidi sitadiriki kuitoa Popote na hata waliotuhisi tulikuwa tunawakatalia.., iwe Faragha au mbele ya hadhira tulitamka Sio Kweli, Hapana, Hakuna Kitu Kama hicho..’ Hayo ndo yalikuwa Majibu Yetu…

“Sasa Umeondoka bila kunipa ruksa juu ya hili Je, niendelee kuitunza hii siri .., na Je, anavyoendelea Kukua akija kuniuliza na nikwambia Mama alisema uwe siri atanielewa Kweli ”..” ?

Wallah Moyo wangu unauma Martha , hukupaswa kuondoka wakati huu, Mapema mno Dah ..!! “Nenda Martha Mwingi Furaha na Ucheshi, Hata Mama Kasema Leo Msiba..:, ‘ jana ulikuwa unatabasamu hadi ulipofumba Macho, “Innalillah Wainnailaih Raajuun ” ..’ Mwenyezi Mungu akupe Kauli thabiti inshaallah.., ‘ Lala salama Martha 🙏

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Mbosso (@mbosso_) on


Story nzima ipo kwenye Website ya Global Radio, Pia Pakua App ya #255GLOBALRADIO Kwenye Google Playstore.


Loading...

Toa comment