The House of Favourite Newspapers

Masogange Ahukumiwa Jela kwa Madawa ya Kulevya, Aachiwa – Video

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa kosa la kutumia madawa ya kulevya aina ya  heroin na Oxazepam..

 

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema kuwa katika ushahidi wa kesi hiyo upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watatu, huku utetezi ukiwa na shahidi mmoja.

 

Mashauri amesema kuwa ameridhishwa pasi na kuacha shaka juu ya ushahidi wa upande wa mashtaka hasa kwa uthibitisho uliotolewa na Mkemia Mkuu wa serikali kwamba mkojo wa mshtakiwa ulikutwa na chembe chembe za dawa za kulevya.

 

Baada ya Masogange kutoa utetezi wake, Hakimu Mashauri amesema kuwa ameusikia utetezi wa mshtakiwa kwamba apewe adhabu ndogo, huku upande wa mashtaka ukitaka apewe adhabu kali.

 

Kosa la kwanza la mtuhumiwa kutumia dawa za kulevya aina ya heroin amehukumiwa miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi milioni moja huku kosa la pili la mtuhumiwa  kutumia dawa aina ya oxazepam amehukumiwa miezi 12 au kulipa faini ya shilingi laki tano.

 

Msanii huyo alikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Februari 15, 2017, akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.

 

Masogange alikuwa miongoni mwa watu maarufu waliotajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati akipambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

 

UPDATES: Msanii Agnes Gerald aka Masogange ameachiwa huru mara baada ya kulipa faini ya Sh milioni 1.5..

Comments are closed.