Masogange laivu na midume miwili hotelini

MASOGANGE5Muuza nyago maarufu Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’.

Hamida Hassan na Gladness Mallya
AIBU jamani! Muuza nyago maarufu Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ametia aibu baada ya kunaswa laivu hotelini akifanya yake na wanaume wawili tofauti, Ijumaa Wikienda linaripoti.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Masogange, tukio hilo lilijiri katika Hoteli ya Lamada iliyopo Mbezi-Beach jijini Dar hivi karibuni baada ya mrembo huyo kutua Bongo akitokea nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ kwenye makao yake yasiyo wazi.

IMG-20151016-WA0024

Akiwa na mmoja kati ya midume hiyo.

Katika picha za tukio hilo, Masogange, akiwa kwenye vazi moja na kwa nyakati tofauti, alikuwa akijiachia kimahaba na wanaume hao, mmoja akitajwa kuwa ni raia wa Uganda.
“Yaani unaambiwa Masogange alikuwa na wanaume hao wawili tofauti bila kujali ataelewekaje… da! Jamani hawa dada zetu nao,” kilisema chanzo hicho.

IMG-20151016-WA0023Baada ya kubwagiwa ‘ubuyu’ huo na picha kutufikia, wanahabari wetu walimwendea hewani Masogange ili atolee ufafanuzi tukio hilo lakini hakupokea simu.

Hata hivyo, waandishi wetu hawakukata tamaa, walimtumia ujumbe mfupi kwa njia ya simu lakini pia hakujibu.


Loading...

Toa comment