The House of Favourite Newspapers

Masomo Yanayohusisha Hesabu Ni Changamoto Kwa Watahiniwa Wa Ununuzi Na Ugavi

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi.

Masomo yanayohusisha hesabu yamekuwa yakiwaangusha watahiniwa wanaofanya mitihani ya bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB).

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza matokeo ya mitihani ya 25 ya bodi hiyo jana jijini Dodoma,  Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kuwa kati ya watahiniwa 1,135 waliofaulu ni 613 sawa na asilimia 54.0 na watahiniwa wengine 474 watarudia somo moja hadi matatu na wengine 48 wamefeli masomo yote katika ngazi mbalimbali.

“Masomo kama ya statistics, Qualitative method na Financial Management hawakufanya vizuri na hii ni kutokana na kutokuhudhuria vituo vya maandalizi na  baadhi ya watahiniwa kudhani uelewa wao ule waliokuwa nao vyuoni wanaweza kaa tu, wakaamka na kwenda kufanya mitihani ya bodi bila kufanya maandalizi hii ndio sababu ya watahiniwa wengi kufeli”, amesema Mbanyi.

Leave A Reply