‘MASTA BATA’ ya NMB Kiboko, Wateja Wabebelea Zawadi Kama Zote!

BENKI ya NMB, leo imetoa zawadi kwa wateja wao ambao wameibuka washindi baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kila wiki ya Shindano la Mastabata.

 

Akizungumza baada ya kupatikana kwa washindi hao, Meneja Mwandamizi wa Kadi wa NMB, Manfred Kayala, alisema washindi hao 20 wamejishindia shilingi laki moja na washindi wengine sita wamekabidhiwa simu za kisasa za Samsung GalaxyS9.

 

Kayala alisema kuwa washindi hao 20, wamefanya jumla kuwa 80 ndani ya mwezi mmoja kwani kila wiki wanapatikana 20 na sasa ni wiki ya nne.

 

Meneja huyo aliongeza kuwa, wataendelea na droo zingine ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, huku droo ya mwisho iliyopewa jina la Grand Finale inatarajiwa kutoa washindi watatu watakaoenda Dubai na wapendwa wao huku NMB ikigharamia kila kitu.

 

“Wateja wetu wa NMB tunapenda kusisitiza kwamba wale wenye kadi za master card tunawahimiza watumie kadi hizo kwani wanaweza kupata zawadi nyingi ikiwemo simu za kisasa kabisa, vilevile unapata nafasi ya kwenda Dubai na kukaa huko kwa siku nne ukiwa na mwenza wako na sisi tutawalipia kila kitu.

 

 

“Lakini kwa wale ambao si wateja wetu, nawasisitiza waweze kujiunga nasi na watumie kadi zao waweze kuwa na nafasi ya kushinda,” alisema Kayala.

Na Mwandishi Wetu.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment