testiingg
The House of Favourite Newspapers

Mastaa 20 Kufanyiwa Tathimini Yanga Baada ya Kichapo cha Mabao 2-1 Dhidi ya Ihefu

0

BENCHI la ufundi la Yanga limeweka wazi kuwa litaufanyia tathimini mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu uliochezwa Uwanja wa Highland Estate ambao ulikuwa ni wa kwanza kupoteza.

Yanga ilikubali kichapo cha mabao 2-1 baada ya kucheza mechi 49 za ligi bila kupoteza. Cedric Kaze, kocha msaidizi wa Yanga alisema kuwa wataufanyia tathimini mchezo huo pamoja na wachezaji wote ambao walihusika kwenye mchezo huo.

Ni nyota 20 walihusika kwenye mchezo huo ikiwa ni pamoja na Diarra Djigui alikaa langoni huku benchi akiwa Aboutwalib Mshery, wengine ni Kibwana Shomari, Lomalisa Mutambara,Dickson Job, Yanick Bangala, Zawad Mauya, Khalid Aucho, Salum Abubakar, ‘Sure Boy’.

Pia Fiston Mayele, Dennis Nkane,Tuisila Kisinda, Bacca, David Bryson, Gael Bigirimana, Dickson Ambundo, Jesus Moloko, Aziz KI, Clement Mzize na Yusuph Athuman walikuwa sehemu ya mchezo huo.

Kaze amesema: “Wenyewe mmemuona wachezaji wote performance, (uwezo) yao haikuwa nzuri.Wale ambao tumecheza nao walikuwa wanahitaji ushindi na kupoteza kwetu kunatupa nguvu ya kujitathimini kwa mechi ambazo zinakuja,”.

#EXCLUSIVE: RESTY AWAMWAGIA SIFA DIAMOND, ZUCHU – ”NAWAPENDA SANA”…

Leave A Reply