MASTAA 6 WAPYA KUPINDUA MEZA YANGA

UKOSEFU wa mechi ngumu na za maana za kimataifa jana kuliiponza Yanga na kujikuta wakilazimisha sare ya usiku ya bao 1-1 mbele ya mashabiki wao kwenye Uwanja wa Taifa.

 

Yanga ilianza kuchapwa lakini ikasawazisha na kwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya Township Rollers ya Botswana ambayo ilikuwa kwenye kambi nzito ya mazoezi nchini Afrika Kusini.

 

Matokeo ya juzi yaliwashtua wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Sibomana ambapo walilazimika kukutana faragha chumbani kwa dakika kadhaa baada ya mchezo huo kumalizika.

 

Lakini habari zinasema kwamba jana Jumapili pia walikuwa na kikao kizito na kocha Mwinyi Zahera huku mkakati ukiwa ni mbinu za kupindua matokeo ya jana
watakapokwenda ugenini.

 

Shujaa wa Yanga katika mechi hiyo ni winga, Patrick Sibomana ambaye amekuwa na kasi ya hali ya juu ya kupachika mabao akifunga mabao nane katika mechi tisa.

 

Kabla ya kufunga penalti ya kusawazisha dakika ya 86, Sibomana raia wa Rwanda alikosa penalti baada ya beki Ofentse Nato kushika mpira akiwa ndani ya boksi. Penalti hiyo ilipanguliwa na kipa wa Rollers, Wagarre Dikago.

Awali, bao pekee la Rollers lilifungwa na Phenyo Serameng kwa shuti dakika ya 7 baada ya kuwatoka mabeki wa Yanga akiwa ndani ya boksi. Yanga walicheza mchezo huo wakiwakosa zaidi ya nyota wao sita kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vibali vya kazi.

 

Kikosi hicho kiliwakosa Kelvin Yondani, Juma Abdul, Andrew Vicent ‘Dante’, kipa wao namba moja Farouk Shikalo, David Molinga Falcao, Abdulazizi Makame na Maybin Kalengo ambao wenyewe wana shida ya kuchelewa kwa leseni.

 

Mashabiki hao wanaamini juu ya kupindua matokeo ugenini kwani huko watakuwa na jeshi lao lote wakiwemo wachezaji ambao hawajacheza kwa sababu mbalimbali.

 

Hata hivyo kwenye mechi hiyo Yanga walipata pigo baada ya beki wake chipukizi mwenye kasi, Paul Godfrey ‘Boxer’ kupata majeraha ya misuli na kuondoshwa
uwanjani akiwa kwenye machela.

 

Katika dakika karibu 60 za mchezo huo timu zote zilicheza zaidi katikati ambako kulikuwa na wachezaji wengi lakini kipindi cha pili, Mwinyi Zahera akawasisitiza wachezaji wake wahamie pembeni ili kutengeneza matokeo na kutumia faida ya nyumbani. Zahera alisema;

 

“Mechi kama hizi ni muhimu sana kushinda nyumbani lakini hata matokeo ya sare ni
mazuri, hakuna aliyeshinda. Sisi tunakwenda kujipanga na ninaamini kwamba tukitimia mechi ijayo tutashinda hata mabao mawili na kuendelea,hii mechi bado iko wazi sana.”

 

Yanga walianza; Metacha Mnata, Paul Godfrey ‘Boxer’, Muharami Issa ‘Marcelo’, Ally Sonso, Lamine Moro, Papy Tshishimbi, Mohammed Issa ‘Banka’, Balama Mapinduzi, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob. na Juma Balinya.


Loading...

Toa comment