The House of Favourite Newspapers

MASTAA BONGO WAISHI KWA NAMBA 9

UKIONA mtu anatukanwa halafu anacheka ujue maisha yake yanaongozwa na namba 9. Uzuri wa namba hii ni kwamba hutoa majibu sahihi kutegemea mtu anaposimama wakati wa kuisoma.

 

Namba 9 ukiigeuza itasomeka 6 na majibu yote ni sahihi; huu ndiyo uajabu wa namba hii ambayo sifa zake hazilingani na nyingine.Mtu anayeishi kwa kutumia kanuni ya namba hii anahitaji umakini mno kumwelewa kwa sababu kuna wakati unaweza kudhani dishi la kichwa limecheza kumbe ameigeuza 9 imekuwa 6 na yote ni majibu sahihi.

 

Kuna kisa kimetokea juzi bungeni; Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku ‘Musukuma’ alisimama na kutamka maneno haya:

“Tasnia ya filamu iko hoi bin- taabani na ndiyo maana unakuta wasanii wetu wa Bongo Muvi hawana kitu, sasa hivi wanategemea misiba wapate michango na kufungua madanguro na kuwa makuwadi kwa wanaume, wako hoi bin- taabani.”

 

Alisema haya wakati akichangia bajeti ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo na kumtahadharisha waziri mwenye dhamana Harrison Mwakyembe ajichunge vinginevyo sanaa itamfia mikononi mwake.

Nakumbusha; kwa miaka mingi tumefanya kazi na wasanii mbalimbali, tumewasaidia wengi kuinuka; nawajua tabia zao na mihemko yao. Umwambie Steve Nyerere amechoka kiasi cha kuendesha maisha yake kwa kupiga michango ya misiba halafu akufurahiye… Weee!!

 

Umwambie Simon Mwakifwamba kwamba anaungaunga maisha kwa kuwatafutia wasanii wenzake wa kike mabwana, halafu aangue kicheko na kuonesha meno yote nje, labda siyo Mwaki-fwamba ninayemfahamu. Kwamba Wema Sepetu, Lulu, Wolper, Kajala, Uwoya uwaambie wanaishi kwa kutegemea kujiuza halafu wasuuzike mioyo yao na kukusifu kuwa umesema lililo jema, hayo ni mageuzi makubwa mno ya namba.

Sikiliza kilichonisha-nganza; nilitaraji kabisa baada ya Musukuma kutamka kuwa wasanii wa Bogo Muvi wako hoi bin taabani na kwamba wanae-ndesha maisha kiujanja-ujanja wangekuwa mbogo, lakini haikuwa hivyo! Matokeo ya kushangaza kabisa walipoambiwa wanaishi kwa kutegemea wenzao wafe ili wachangishe fedha za rambirambi wengi walifurahi na kuitisha mkutano kujadiliana namna ya kumpongeza Musukuma kwa kuwatetea bungeni kwamba wako hoi.

 

Haikutosha hiyo; wakapanga safari ya kumfuata Dodoma ili kumpa mkono wa pongezi shujaa mpigania hali zao Musukuma; jambo hili limenishangaza sana. Nikajiuliza Bongo Muvi wamekuwaje hawa; wanadhalilishwa namna hii halafu wanafurahia? Baadaye nikakumbuka wamebadilisha mkao sasa wanaisoma namba 9 kama 6 na hakika wako sahihi.

 

Maana kipindi tunawaandikia habari kuwaambia ‘maisha yao yamejaa giza’ walituona kama wendawazimu kwa sababu walikuwa wanaitazama 6 kama 9.

Leo wasanii wetu wamegeuka wenyewe; wanaitazama 9 kama 6 na kusema kweli wako sahihi. Hawapaswi kuchekwa wala kudhar-aulika. Ajabu iko hivi; Bodi ya Filamu nchini iliposikia maneno ya Musukuma ilikuja juu ikasema: “Wasanii wamedh-alilishwa sana.”

 

Bodi ikakataa kabisa Steve Nyerere kuendesha maisha yake kwa kutegemea fedha za misiba, ikagoma Wema kufungua madanguro na kujiuza kwa wanaume na kumtaka Musukuma awaangukie wasanii wa Bongo Muvi kwa kuwatusi. Wanao-tetewa walikubali? Ndiyo kwanza waliunga mkono udhalilishaji huo kwa kusema: “Unafaa sana.” Na mdha-lilishaji wakamuita shujaa wao.

Kama hilo halitoshi nilipohojiana na baadhi yao walisema; yule anayewatetea kwa maana ya bodi ndiyo hawamtaki kabisa na kwamba wanataka iondolewe haraka iwezekanavyo. Ama kweli haya ndiyo maajabu ya namba 9 inategemea mahali uliposimama. Walipochukia tulipowaambia fedha wanazotumia na maisha wanayoishi siyo safi walitubeza; narudia kusema makosa hayakuwa yao ni mahali walipokuwa wamesimama wakati wakiisoma namba 9.

 

Nakumbuka tuliwahi kuandika habari inayowatuhumu baadhi ya wasanii wa kike kuendesha maisha kwa kujiuza, waligeuka mbogo; hata pale tulipowanasa laivu baadhi yao kwenye mtego wa kujiuza bado hatukueleweka, tuliambiwa tunawachafua. Leo kiko wapi? Wanaambiwa tena bila ushahidi kuwa wamefungua mada-nguro, wana-jiuza wen-yewe wanapiga makofi.

Niseme; kilichowaponza wasanii hao anaowatetea Musukuma kuwa hoi ni kuigeuza sanaa kuwa uwanja wa kujulikana kuendesha maisha ya ujanjaujanja. Wasichana walikuwa wakikimbilia kwenye sanaa ya maigizo siyo iwalipe bali iwape jina mjini ili ‘wajiuze’. Kazi yoyote usipoithamini nayo haitakuthamini kamwe, lazima ikuangushe kama ambavyo Bongo Muvi wameanguka.

 

Nawashauri; bado wanayo nafasi wajipange na waiheshimu sanaa kama wenzao Wakorea wanavyofanya nayo itawaweka juu kileleni. Wasipofanya hivyo wataishia kudhalilishwa kwa maneno na kuwapisha wenye juhudi zao Wakorea wakiteka soko walilokuwa wameli-shikilia

Comments are closed.