The House of Favourite Newspapers

Mastaa hawa muziki damu, Filamu Damu

0

12237083_1520711531575289_1965832897_nDiana Exavery ‘Malaika’.

MUZIKI wa Bongo Fleva kwa sasa upo kwenye ‘ubora wake’ na hilo halina ubishi. Wapo wanamuziki wanaofanya poa kama vile Diamond, Ali Kiba, Chegge, AY, MwanaFA, Vee Money, Joh Makini na wengine wengi.

Lakini ukiachana na Bongo Fleva, filamu nazo bado zinakubalika nchini japokuwa si sana. Katika sanaa zote hizi mbili (filamu na muziki) wapo wasanii ambao tunaweza kuwaita kwao damudamu na vitu hivi viwili yaani Muziki Damu na Filamu Damu.
Katika makala haya yanachambua baadhi ya wasanii hao;

hemed2Hemed Suleiman.

Hemed
Hemed Suleiman ni mmoja kati ya wasanii wa filamu wanaotikisa nchini. Miongoni mwa filamu alizocheza ni Confusion akiwa na Lulu, Nisha, Diana Kimari pamoja na Filamu ya Bad Girl akiwa na Rose Ndauka. Kwa upande wa muziki kwake upo kwenye damu na amekuwa akitoa wimbo mpya mara tatu hadi nne kwa mwaka. Kwa sasa anabamba na Ngoma ya Imebaki Stori.

Kidoa
Asha Salum ‘Kidoa’ anasimama kwa upande wa muziki kama ‘muuza nyago’ (Video Queen) japokuwa kuimba yupo vizuri lakini bado hajatoa ngoma ya peke yake. Kidoa alifahamika zaidi kwenye Video ya Wimbo wa Akadumba ulioimbwa na Nay wa Mitego. Kwa upande wa filamu kwake ni damudamu na ameshiriki filamu chache ikiwemo ya Kifaacho Mtu akiwa na Riyama Ally.

Malaika
Jina lake halisi ni Diana Exavery. Kwake muziki na filamu ni kati ya vitu vilivyopo kwenye damu na kwa upande wa filamu zipo baadhi ya alizowahi kushiriki ikiwa ni pamoja na Mrembo Kikojozi ya Aunt Ezekiel na Mtunisi. Kwa upande wa muziki anafanya poa kuanzia Ngoma ya Mwamtumu hadi ya sasa ambayo ni Zogo.

Linex-LINEX
Sunday Mjeda ‘Linex’ ni mkali wa nyimbo za hisia kwa upande wa Bongo Fleva. Linex ambaye kwa sasa anabamba na Ngoma ya Kwa Hela pia kwa upande wa filamu kwake ipo kwenye damu na miongoni mwa filamu alizofanya vizuri ni pamoja na Mwajuma Nipe akiwa na Aunt Ezekiel pamoja na King Majuto.

Gigy Money
Gift Stanford ama Gigy Money kwa jina la kisanii ni mmoja kati ya mavideo queen wanaotikisa Bongo akiwa ametokelezea kwenye video kadhaa kama vile Siachani Nawe ya Barakak Da Prince na Bishoo ya Quick Racka akiwa na Young Dee.

Kwa upande wa filamu pia ipo kwenye damu kwani hivi karibuni alitangaza kuingia rasmi na kwa sasa yupo chimbo kuibuka na filamu mpya ambayo jina lake halijawekwa ‘kwenye dawati’.

Wapo pia wasanii wengine ambao muziki na filamu kwao vipo katika damu kama vile Kingwendu, Shilole, Snura, Sabby Angel, 20 Percent na wengine wengi.

Leave A Reply