The House of Favourite Newspapers

Mastaa Hawa Wamekopi na Kupesti Hadi Nywele?

0

Harmonize-1Harmonize

Andrew Carlos

MASTAA wa Bongo bwana! Baada ya kukopi na kupesti staili ya kuimba na biti zao nyingi kufanana na za Sauz na Nigeria ni kama wamehamia kwenye staili mpya ya usukwaji nywele inayotumika hasa kwa mastaa nchini Marekani.

Ukiwaangalia muonekano wa vichwa vyao, baadhi ya mastaa hawa wakiongozwa na Jux, Romy Jones, Harmonize na wengine kibao utagundua kuna kitu wamekopi na kupesti kutoka kwa mastaa wa mbele ambao ni Chris Brown, Post Malone, The Game, Omario na wengineo

Inaitwaje?

Staili hii iliyotokea kujizolea umaarufu mkubwa kwa mastaa mbalimbali hususan wa muziki inajulikana kama Dutch Braid japokuwa chimbuko hasa la staili hii lilikuwa likijulikana kama French Braid.

omarions-new-hairOmarion

Staili hii ipoje?

Usukwaji wake huwa wa nywele kuanzia njia mbili kubwa kisha kwa nyuma inafungwa ama kuachiwa mikia.

Mastaa wengi wa kike kama Kim Kardashian, Karrueche na wengineo wanapenda kusuka njia mbili ndefu za kuacha mkia ukining’inia na kwa upande wa mastaa wa kiume, pande zote za pembeni hunyoa na katikati husuka njia mbili ama tatu kisha huzifunga kwa nyuma.

postmalone2.jpegPost Malone

Staa huyu wa muziki nchini Marekani ambaye pia ni rafiki mkubwa wa Justin Bieber, amekuwa akibadili staili ya nywele zake mara kwa mara.

Ukicheki baadhi ya video zake za hivi karibuni alizofanya na wakali kama Young Thug, 50 Cent na Kanye West kichwani kwake utamuona katika muonekano wa Ki-dutch.

the gameThe Game

Mei mwaka huu, kupitia ukurasa wake wa Instagram, kwa mara ya kwanza rapper The Game aliitambulisha staili hii ya Duth kwa mashabiki wake.

Rapa huyu kutoka Los Angeles, Marekani aliiweka picha mtandaoni akiwa saluni katika matengenezo ya staili ya Dutch na baada ya hapo alipewa shavu la kutosha kutoka kwa mashabiki.

chris-brown-new-hairstyle-corn-rows-ftrChris Brown

Mkali huyu wa R&B kwa miaka mingi amekuwa hatabiriki katika staili zake za nywele lakini baada ya staili hii kuteka mastaa wengi naye amekuwa miongoni mwao.

Chris ambaye ni baba wa mtoto mmoja, Royalty amekuwa akitupia picha zake mitandaoni zikimuonesha katika muonekano wa Ki-dutch lakini kwa staili mbalimbali.

JUXCJux

Kuonesha kuwa mastaa wa Bongo hawapitwi na kitu katika kukopi na kupesti, staa wa Ngoma ya Wivu, Jux amekuwa miongoni mwa mastaa Bongo waliotekwa na staili hii.

Jux ameonekana kula sahani moja na Chris Brown. Mara ya kwanza Chris alitengeneza staili hii ya Dutch kizamani kwa kuning’iniza nywele mbili mbele na nyuma kubana, Jux alipoona akakopi na kupesti.

Chris akabadili staili hiyo na kunyoa za pembeni, nyuma akizibana. Jux kuona hivyo naye akaiga tena ambayo ndiyo anayo hadi sasa.

Harmonize

Staa huyu anayebamba na Ngoma ya Matatizo, baada ya kuongeza michoro kadhaa mwilini mwake (tattoo), ameamua kubadili na staili ya nywele.

Alichokifanya kichwani kwake, amejaribu naye kukopi na kupesti staili ya Dutch ambapo kwa sasa amekuwa akitupia picha nyingi na vipande vya video akiinamisha kichwa ili mashabiki wake waione staili hiyo mpya ya nywele.

Romy Jones

Hivi karibuni, binamu na DJ wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond, Romy Jones katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Next Door, jijini Dar aliingia na sapraizi kichwani kwake akiwa katika muonekano wa Ki-dutch.

Kama ulivyo muonekano wa nywele kwa sasa wa Omario, Chris Brown na The Game kwa Rommy hakuna tofauti yoyote kwani naye amekopi na kupesti tu.

Leave A Reply